Watumishi 15 wa Mungu watekwa

HomeKimataifa

Watumishi 15 wa Mungu watekwa

Watumishi wa Mungu wapatao 15 na familia zao wamevamiwa na kutekwa  na kundi la wahalifu nchini Haiti eneo la Port-au- Prince walipoenda kutembelea kituo cha watoto yatima kutoa misaada mbalimbali. Ikumbukwe kwamba nchi ya Haiti ilikumbwa na tetemeko kubwa ardhi lilioacha idadi kubwa ya wananchi wakiwa hawana makazi ya kudumu na kukosa mahitaji.

Tangu kuuawa kwa Rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise Julai mwaka huu, kumekuwa na matukio mbalimbali ya utekaji ambapo wahuni wamekuwa wakitumia kukosekana kwa ulinzi kama njia ya kufanya uhalifu.

Polisi nchini humo wamesema, watumishi hao wa Mungu wametekwa muda mfupi baada ya kutoka mji wa Croix-des-Bouquets na kwa sasa wanaendelea kushikiliwa na wahuni hao huku serikali ya Marekani haijatoa tamko lolote kuhusiana na kutekwa kwa raia wake huku ikisisitiza kuwa bado inaendelea kufuatilia suala hilo.

Wananchi wengi wa Haiti wanaiomba serikali ya Marekani kutuma vikosi vya ulinzi ili kuimarisha usalama jambo ambalo Rais Biden amekuwa mzito kulikubali.

error: Content is protected !!