Waziri Kombo Amkabidhi Rais Museveni Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Samia

HomeKimataifa

Waziri Kombo Amkabidhi Rais Museveni Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Samia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe Malumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Gen. Yoweri Kaguta Museveni Entebbe, Uganda. Tarehe 13 Mei, 2025

Waziri Kombo aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Maj. Jen. Paul Kisesa Simuli.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Kombo ametembelea majengo ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda yakijumuisha makazi ya awali ya Balozi yaliyopo Kololo.

Aidha, Waziri Kombo alihitimisha ziara yake kwa kufanya kikao kazi na Watumishi wa Ubalozi wakiongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Mej. Jen.  Paul Kisesa Simuli, ambapo aliweka mkazo katika masuala muhimu ikiwa ni pamoja na utendaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za Serikali, pamoja na kuibua fursa nyingi zilizopo kati ya Tanzania na Uganda.

error: Content is protected !!