Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, amenusurika kuuawa katika jaribio la mauaji katika mashambulizi yaliyofanywa kwa kutumia ndege inayorushwa bila ya rubani (Drone) Katika shambulio hilo lililolenga makazi ya Waziri Mkuu al-Kadhimi, yaliyopo katika eneo mashuhuri linalotambulika kama ukanda wa kijani jijini Bahgdad
Baada ya kushindika kwa tukio hilo Waziri Mkuu alijitokeza hadharani na kueleA kuwa yuko salama na anaendelea vizuri huku akitoa wito kwa watu wote kuwa watulivu na wavumilivu hasa katika kipindi hiki. Ikumbukwe kwamba nchi ya Iraq kwa sababu imegubikwa na maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa Bunge uliofanyika mwezi uliopita ambao makundi yenye kuiunga mkono Iran yalishindwa vibaya.