Wenje: CHADEMA ilikimbia uchaguzi kwa kuogopa ushindani

HomeKitaifa

Wenje: CHADEMA ilikimbia uchaguzi kwa kuogopa ushindani

Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana na kiongozi wa CHADEMA, sasa Kada wa CCM, Ezekiel Wenje, amesema ni hatari kwa taifa kuwa na kiongozi wa chama cha siasa anayesema yuko tayari kufa, akisisitiza kuwa CHADEMA ilisusia uchaguzi kwa kuogopa ushindani.

Akizungumza Muleba, Kagera mbele ya Rais na Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wenje alisema CHADEMA walijiondoa kwenye uchaguzi licha ya serikali ya awamu ya sita kutekeleza mapendekezo yao kuhusu marekebisho ya mifumo na sheria za uchaguzi.

Wenje alimpongeza Dkt. Samia kwa kuimarisha maridhiano ya kisiasa, kufungua mikutano ya hadhara, na kufanya mabadiliko muhimu ya uchaguzi, ikiwemo kuondoa kipengele cha “kupita bila kupingwa” na kuzuia wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi mkuu.

error: Content is protected !!