Kwa wafuatiliaji na wadau mbalimbali wa tasnia ya mitindo duniani, tukio la Met Gala, sio kitu kigeni masikioni kwao. Ukubwa wa tukio hili unafananishwa kwa ukaribu na tukio la ugawaji wa tuzo za filamu za Oscars, mara nyingine tukio hili huitwa Oscar’s za Mitindo.
Mwaka huu tukio hilo lilihudhuriwa na watu maarufu wengi na kama inavyojulikana kwamba watu hutoa fedha ili kuweza kupata mwaliko, lakini sasa imekua tofauti kwa sababu kuna baadhi ya wasanii na watu maarufu ambao hawakupata mwaliko huo mmoja wapo akiwa rapa Wiz Khalifa.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Wiz Khalifa aliweka wazi sababu ya yeye kutokuwepo katika tukio hilo kwamba waandaaji walimnyima mualiko wakihofia kwamba anaweza kuvuta bangi ukumbini.
They were scared of me smoking on the red carpet or at the event so no met gala. I don’t blame em but weed is legal dude, sheesh.
— Wiz Khalifa (@wizkhalifa) May 3, 2022
Ifahamike kwamba rapa huyo ambaye huenda baada ya Snoop Dogg, anashika nafasi ya pili kwa kupenda kuvunta ganja aliamua kuwekeza kwenye biashara ya mmea, Khalifa Kush.