Huduma za Twitter kulipiwa

HomeBurudani

Huduma za Twitter kulipiwa

Bilionea Elon Musk ambaye ndiyo mmiliki wa mtandao wa Twitter ameshikilia msimamo wake wa kuleta mabadiliko kwenye mtandao huo ikiwemo kulipia huduma hiyo.

Wiki iliyopita, Musk aliinunua Twitter kwa dola bilioni 44 sawa na trilioni 102.05 za Kitanzania.

Amesema imefikia pahala ambapo wale wanaofanya biashara kupitia twitter pamoja na akaunti za serikali kuanza kulipia kutumia mtandao huo.

Musk ameeleza kuwa malipo hayo hayatowahusisha watumiaji wa kawaida wa mtandao huo.

Twitter itaendelea kuwa bure kwa watumiaji wa kawaida, lakini itagharimu kidogo kwa watumiaji wa kibiashara/serikali,” ameandika hiyo kwenye mtandao huo.

Musk anasema kuwa hiyo ni hatua tu kwa mabadilikomengi yanayokuja kwenye mtandao huo ikiwemo kitufe cha ku ‘undo tweet’ yaani kuifuta mara moja tweet kabla haijachapwa mtandaoni.

Tetesi zainasema kuwa Musk ameongea na baadhi ya wawekezaji akisema kuwa hana mpango wa kuimiliki Twitter kwa muda mrefu na ataanza kuuza hisa za kampuni hiyo ndani ya miaka hii mitatu.

Musk ndiye tajiri namba moja duniani. Hadi kufikia Aprili 6, Business Insider wanamtaja Musk kuwa na thamani ya zaidi ya dolo za kimarekani bilioni 300.

error: Content is protected !!