Mwenyekiti CCM Shinyanga ataka bango la Ndugai ling’olewe

HomeKitaifa

Mwenyekiti CCM Shinyanga ataka bango la Ndugai ling’olewe

Mwenyekiti wa CCM Shinyanga, Khamis Mgeja amesema kwamba kitendo kilichofanywa na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Job Ndugaicha kuikosoa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sawa na kuinajisi nchi hivyo kuendelea kuonekana jina lake kwenye majengo ya umma ni kuwatia kichefuchefu watanzania.

“Kwa makosa aliyofanya Ndugai, kwa kweli hata kama kutakuwa na kumbukumbu zake katika majengo ya umma, ziondolewe mara moja, nchi zingine hata mabango, sanamau za viongozi wanaofanya mambo ya hovyo huwa yanaharibiwa na mengi huvunjwa kwa hasira na wananchi,” alisema Mgeja.

Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza Watanzania kwa jinsi walivyoonesha nguvu ya umma na mapenzi ya dhati juu ya Rais Samia Suluhu huku akisema kwamba hii imeonyesha kwamba watanzania wakiamua jambo wanaweza kumng’oa mtu kokote aliko, hata kama ni mbabe mwenye jeuri mfano wa Ndugai, na kushauri wafuasi wake pia wachukue hatua alizochukua bosi wao.

“Binafsi nimefurahishwa na kitendo cha Ndugai kutangaza kujiuzulu wadhifa wake wa uspika kwa Bunge, kwa kweli kitendo cha kudai nchi yetu inaweza kupigwa mnada, kutokana na ukubwa wa madeni kiliwashtua watanzania wengi,” alisema Mageja.

Pia Mgeja alisema busara itumike kwa kuondoa majina ya Ndugai popote yalipo mfano Dodoma ambako kuna jina lake kwenye soko la kisasa lililopewa jina la Ndugai na kusema wafuasi wake wajitathimini haraka na ikiwezekana wachukue uamuzi wa kujiuzulu kama aliochukua nahodha wao(Ndugai) huku akimtaja mmoja Humphrey Polepole kama mmoja wao.

error: Content is protected !!