Iyobo aweke wazi kupewa magari 10 na Diamond Platnumz

HomeBurudani

Iyobo aweke wazi kupewa magari 10 na Diamond Platnumz

Dansa maarufu nchini Tanzania Mose Iyobo amefunguka na kuweka wazi kwamba msanii maarufu na mmiliki wa lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz amewahi kumzawadia magari zaidi ya kumi tangu 2010 lakini hajawahi kuonyesha mtandaoni kwani bado anahisi haujafika muda muafaka wa yeye kutoa shukurani kwa bosi wake huyo.

“Mimi nimeanza kupewa magari tokea 2010 ni vile tu sijawahi kusema asante Diamond kwa gari kwa sababu nahisi bado haijafikia siku ya kusema asante Simba hichi nina stahili, sijawahi kusema asante kwa gari…. Magari yanafika kumi la mwisho nimeuza juzi hapa,” alisema Iyobo.

Iyobo pia amesema Diamond amemfanyia mambo mengi sana makubwa huku akiongezea kwamba kama anahitaji siku yakutoa shukurani aandaliwe kipindi maalumu cha Shukurani za Iyobo kwa Diamond Platnumz.

Akiongea kama kiongozi wa madansa wa Diamond Platnumz amesema kwamba safari yao ya kucheza walianza wakiwa wanne na baadae kuongeza wawili kukamilisha idadi ya jumla watu sita ambao wapo mpaka sasa na ndio madansa maarufu nchini.

error: Content is protected !!