Joh Makini amtolea uvivu Sallam SK

HomeBurudani

Joh Makini amtolea uvivu Sallam SK

Moja kati ya nyimbo kubwa ambazo Joh Makini amewahi kufanya ni pamoja na “Don’t bother” ambayo alimshikirisha msanii kutoka Afrika Kusini maarufu kama A.K.A. Wimbo huo umeibua mjadala katika ukurasa wa Twitter baada ya meneja wa Diamond Platnumz maarufu kama Sallam SK kuandika kwenye ukurasa wake kuwa yeye ndio aliunganisha wawili hao kufanya nyimbo bila malipo yoyote.

Joh Makini alikuja kujibu kwa ku-comment kwenye hiyo post na kusema aelezee ameunganisha vipi kwani alipambana sana kukwamisha wimbo huo usifanyike.

“Aelezee aliunganisha vipi yeye sio chanzo cha hiyo collabo, kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki wa Pili na G Nako Warawara lakini waliomleta walikua hawataki itokee”.

“Muarabu alipambana sana kukwamisha hii basi tu Mwenyezi Mungu hajawahi kushindwa” ameandika Joh Makini

error: Content is protected !!