Ray C: “Nahisi harufu ya kifo, bifu ya Harmonize na Diamond”

HomeBurudani

Ray C: “Nahisi harufu ya kifo, bifu ya Harmonize na Diamond”

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchi Tanzania Rehema Chalamila maarufu kwa jina la kisanii Ray C amefunguka na kusema kinachoendelea kati ya Harmonize na Diamond sio bifu dogo bali ni vita kubwa na pia anahofia wawili hao watakuja kuchukua hatua mbaya zaidi kama wataendelea hivi miaka ijayo.

“Mtakuja kutoana roho wallah nawaambia na naongea sio kuwaambia nini chakufanya hapana bali naongea tu kama dada na msanii mwenzenu, mnahitaji kumalize hiki kitu sababu naona kabisa kwa upeo wangu mdogo baada ya miaka miwili au mitatu mtakuja kuuana,” amesema Ray C.

Ray C amesema ikiwezekana serikali iingilie kati suala la wasanii hawa wawili iliwaweze kumalizana na kuawatuliza kwani ni watu wanaoipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuwakilisha Taifa nje vizuri hivyo ni bora wakatulizwa mapema kabla ya matokeo mabaya kuja baadae.

error: Content is protected !!