Diamond ashauriwa kuacha Muziki

HomeBurudani

Diamond ashauriwa kuacha Muziki

Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na stori kuwa msanii Diamond Platnumz sasa hivi akitoa nyimbo hazibambi sana kwa ilivyokuwa siku za nyuma. Pengine hii imeweza kutokana na ushindani sokoni au Platnumz ameanza kuridhika kwa mafanikio aliyopata hivyo kupunguza kujituma kwenye muziki.

Kwa sasa msanii anayejiita namba moja nchini, Harmonize anaonekana kutishia kutaka kuchukua ngome ya Diamond Platnumz, Harmonize tangu ajitoe label ya WCB na kuanzisha Konde Ganga amekuwa na moto wa kuotea mbali.

Watu wameanza kusema sasa Diamond Platnumz anaonekana kuwekeza sana kweny mavazi kuliko muziki, hivyo watu wamemshauri kuwa ni bora akafungua sasa kampuni ya mitindo kwani anafanya vyema sana kwenye sekta
hiyo.

Shabiki Hussein Bodea amenukuliwa na Gazeti la “LA JIJI” akiongea maneno hayo. Hussein Bodea aliongeza kuwa Diamond afanye utaratibu wa kuungana na Flaviana Matata ampe uzoefu kwenye sekta hiyo.

Baada ya kuongea na mashabiki kadhaa wa WCB, walionekana kukerwa sana na kauli hiyo na kusema kuwa, bila Diamond Platnumz leo hii pasingekuwa na Harmonize, hata kama angekuwepo, basi sio huyu tunayemjua.

Wewe ukiwa kama msomaji wetu wa clickhabari, unadhani ni kweli Diamond Platnumz amefifia kwenye muziki na ahamishie nguvu kwenye fasheni kama Hussein Bodea anavyosema?

error: Content is protected !!