Wanne wafariki, 17 wajeruhiwa baada ya ghorofa kudondoka Goba

HomeKitaifa

Wanne wafariki, 17 wajeruhiwa baada ya ghorofa kudondoka Goba

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amethibitisha vifo vya watu wanne na wengine 17 kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ghorofa lililokuwa linajengwa kuporomoka na kuangukia nyumba za majirani katika eneo la Goba jijini Dar es Salaam.

“Wanaume wawili ni mafundi waliokuwa wanajenga kwenye jengo hilo na wanawake wawili ni wakazi wa eneo hilo. Mpaka sasa Jeshi la polisi na zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi viko katika eneo hili kwa ajili ya kuendelea na hatua ya kuhakikisha waliojeruhiwa ni hao tu au kuna ziada. Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala. Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mloganzila” alisema Kheri James.

> Sababu 5 zinazoweza kupelekea jengo la ghorofa kuporomoka

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo amewataka wananchi kutosogelea eneo hilo kwa kile alichosema kuwa jengo hili bado limekaa katika mkao wa kuanguka zaidi na zaidi, hata hivyo bado chanzo cha kudondoka kwa ghorofa hilo lililokuwa likijengwa kwa ajili ya shughuli za biashara hakijajulikana.

 

error: Content is protected !!