Simba SC wapo tayari kwa ajili ya Sensa

HomeBurudani

Simba SC wapo tayari kwa ajili ya Sensa

Wachezaji wa Klabu ya Simba SC leo wakiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea tamasha kubwa la SIMBA DAY ambapo wanatarajiwa kucheza dhidi ya Mabingwa wa Soka Ligi Kuu ya Ethiopia, klabu ya St. George SC wametumia muda wao kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la Sensa la Agosti 23, 2022.

 

Wachezaji hao wakiongozwa na Kapteni John Bocco, wameungana na Shomari Kapombe, Aishi Manula, Erasto Nyoni na wazawa wengine kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa wako tayari kuhesabiwa.
“Sisi wachezaji wa Simba SC tunapenda kuwahamasisha watanzania wajitokeze kuhesabiwa kwani ni muhimu kwa maendeleo na mipango ya nchi yetu, tumuunge mkono Rais Samia katika zoezi hili,”amesema Shomari Kapombe Beki wa kulia wa Simba.
Naye Clatous Chama amewaasa watanzania kujitokeza kuhesabiwa kwani zoezi hilo hufanyika nchi zote ili kuweka utaratibu mzuri wa maendeleo ya nchi.
error: Content is protected !!