Jack wa Jux aachiwa huru

HomeBurudani

Jack wa Jux aachiwa huru

Mrembo wa Tanzania, Jackie Cliff ambaye alifungwa gerezani nchini China baada ya kukamatwa Disemba 19, 2013 akijaribu kuingiza dawa za kulevya aina ya heroini zilizokuwa na kilogramu 1.1 nchini humo ametoka jela baada ya kutumikia kifungo cha miaka 8.

Mrembo huyo ameonyesha yupo huru kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuwataarifu mashabiki zake kuanza kumfuatilia kupitia ukurasa wake mpya anaopatikana kwa jina la @ms.jackiecliff .

Jackie aliwahi kuwa video vixen maarufu sana na mpenzi wa msanii wa bongo fleva Juma Jux na mwanamuziki huyo kumuimbia wimbo wa “Nitasubiri” lakini baadae wawili hao waliachana baada ya Jux kuanza mahusiano na Vanessa Mdee ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani na mpenzi wake mpya Rotimi.

Mashabiki wa wamefurahishwa sana na kuachiwa kwake na wamemkaribisha uraiani tena kwa mara nyingine.

error: Content is protected !!