Biashara ya muziki haina faida bila ‘Beefs’, kwanini?

HomeBurudani

Biashara ya muziki haina faida bila ‘Beefs’, kwanini?

Neno ‘Beef’ ni neno la mtaani au neno ambalo sio rasmi kwenye lugha ya Kingereza lenye maana ya kuonesha/kuwa chuki au kutokupenda kitu kitu fulani. Katika uga wa muziki duniani neno beef ni neno maarufu sana miongoni mwa wasanii. Kwa mfano moja ya Beef maarufu kuwahi kutokea kwenye muziki duniani ni kati ya Notorious B.I.G na Tupac, beef ambalo halikuwa na mwisho mzuri kwani wasanii wote hawa walipoteza maisha katika vipindi tofauti na vifo vyao vilihusishwa moja kwa moja na ugomvi waliokuwa nao.

Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia beef kati wasanii mbalimbali katikam mataifa tofauti, mfano Beef kati ya msanii Davido na Wizkid wote kutoka nchini Nigeria.

Kwenye hili na mikasa na ugomvi miongoni mwa wasanii, wengi hudhani kwamba matokeo kama haya yana matokea hasi kwenye maisha ya wasanii, lakini wanasahau usemi maarufu wa kwamba kila jambo lina pande mbili, upande mbaya na upande mzuri.

Beefs au migogoro miongi mwa wasanii inaweza kuwa na faida kubwa sana kibishara kwa wasanii kama migogoro hiyo itatumika vizuri. Zifuatazo ni faida za beefs kwenye biashara ya muziki.

1. Beefs zinafanya wasanii kuongeza juhudi kwenye kazi
Ingawa mara nyingine mgogoro miongoni mwa wasanii inaweza isiwe na uhusiano wowote na muziki wao, lakini mara nyingi tunaona kuwa wasanii waliomo kwenye mgogoro hulinganishwa kazi zao na bashabiki zao, hivyo basi, hali ya kufananishwa husababisa ushindani. Hali hii huwafanya wasanii waongeze jitihada za ari za kupambana zaidi kwenye kazi zao na hii huongeza ladha na chachu kwenye kiwanda cha muziki.

> Zijue faida na hasara za msanii kuwa chini ya Record Label

> Wasanii watano waliowahi kuteswa na mikaba mibovu, ya Record Label

> Diamond ashauriwa kuacha muziki

2. Beefs zinavuta mashabiki zaidi
Amini usiamini kwamba, biashara ya muziki ni biashara kama zilivyo biashara nyingine, na hata biashara hii ina mipango na mikakati ya kuyafikia mafanikio vilevile. Wapo wasanii duniani ambao wamelazimika hadi kutengeneza beefs za uwongo ilimradi wapate kufuatiliwa na kupatilizwa na shabiki zao. Bahati mbaya zaidi jamii tuliyonayo inapenda kusikia habari mbaya kuliko nzuri, kuna mashabiki wataingia kusikiliza nyimbo kwa sababu tu wamesikia msanii fulani amemtusi au kusema vibaya msanii mwingine. Hali hii huongeza mashabiki na mvuto kwenye kiwanda cha muziki.

3. Beefs ni aina nyingine ya burudani
Burudani huja kwa namna nyingi, umeshawahi kuona watu wanalipia viingilio kutizama watu wengine wakipigana kiasi cha kutaka kuuwana, au mtu anatoka na kutembea umbali mrefu kufuata kushuhudia ugomvi, hii yote ni namna ambayo mtu anataka kuridhisha nafsi yake. Ingawa si kila vurugu inaweza kufuatiliwa au kupendwa na watu, ila kwa watu maarufu inakuwa tofauti. Hivi leo watu maarufu wanapobishana na kutupiana maneno mtandaoni, watu hufuatilia na kuburudika.

Kwa kuhimitimisha, sio lazima kuwa na Beefs kwenye muziki ili mziki wetu uende mbali zaidi, lakini kama Beefs hizo zitatumika vizuri kwenye kiwanda chetu cha muziki, basi zinaweza kupeleka mziki wetu mbali zaidi.

 

error: Content is protected !!