Exclusive: Harmonize ndani ya penzi jipya, mcheki hapa

HomeBurudani

Exclusive: Harmonize ndani ya penzi jipya, mcheki hapa

Msaani na mmiliki wa lebo ya muziki ya Konde Gang kutoka nchini Tanzania, Rajab Abdul maarufu kama Harmonize amemuonyesha rasmi mpenzi wake mpya Briana mrembo kutoka nchini Australia ambaye kwa sasa amemlazimu kukwea pipa na kumfuata mpenzi wake Harmonize ambaye nayeye yupo Marekani kwa shughuli zake za kimuziki.

Hivi karibuni Harmonize ametoka kuachana na Kajala ingawa mahusiano yao hayakudumu kwa muda mrefu lakini alikiri kwamba kati ya wanawake wote aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano Kajala ndiye aliyempenda kwa dhati na kumuomba msamaha kwa yale yaliyotokea mpaka kuvunjika kwa penzi lao miezi michache iliyopita.

Kabla Harmonize kumuonyesha mpenzi wake huyu wa sasa aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba kwa sasa anataka atulie na mpenzi wake wa maisha hivyo kuna baadhi ya watu ataachana kuwafatilia, Ikimbukwe Harmonize amewahi kuwa kwenye mahusiano na mwigizaji wa bongo muvi Jackline Wolper, mrembo Sarah Michelotti, Kajala na sasa Briana.

error: Content is protected !!