Mbaroni kwa kutaka kuuza ardhi ya Rais wa Kenya

HomeKimataifa

Mbaroni kwa kutaka kuuza ardhi ya Rais wa Kenya

Watu wanne wamewekwa kizuizini na mahakama ya Nairobi kwa shutuma za kupanga njama za kuuza ardhi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta huko Karen nchini humo.
Watuhumiwa hao ni Mohamed Muhammud, James Opere, Jonah Tuuko na Samakin Lesingiran.

Mwendesha mashtaka wa upande wa serikali ameomba watuhumiwa hao kuendelea kuwekwa kizuizini kwa siku saba  ili kuendelea kuchunguza hati bandia ambazo walizitengeza kwa ajili ya kuuzia kiwanja hiko.

Wakili wa utetezi Danstan Omari anayewawakilisha Opere na Tuuko hata hivyo aliteta kuwa upande wa mashtaka unafahamu kuwa ardhi hiyo ni ya Rais na hafai kuficha utambulisho wake ili kuwaadhibu washukiwa.

Lakini pia Omari alipinga madai kuwa watuhumiwa hao walivamia ardhi hiyo kwa nia ya kuiuza walikamatwa kimakosa.

“Hawa ni watu wadogo ambao hawakuweza kupata ardhi inayomilikiwa na rais kwa sababu inalindwa kote. Ni watu ambao walikuwa wanatembea tu kando ya barabara karibu na ardhi hiyo na walikamatwa kimakosa kwa tuhuma kwamba walikuwa wanakagua vinara,” alisema Omari.

Bado kuna sintofahamu juu ya mmiliki halali wa ardhi hiyo kutokana na mawakili katika kesi hiyo kutofautiana, wengine wakisema ni ya Rais na wengine wakidai ni mali ya mwanasiasa mashuhuri ambaye hataki kujulikana.

Pamoja na hayo hakimu Kamau alikubaliana na Omari akisema kuwa kuzuiliwa kwa washukiwa hao kwa siku saba ni kuwakosesha haki yao jambo baadae lilipelekea kuachiwa kwa dhamana ya Tsh 611,420.

error: Content is protected !!