Wasafi TV wapewa kibano na TCRA

HomeBurudani

Wasafi TV wapewa kibano na TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekipiga faini ya Sh milioni mbili kituo cha Televisheni cha Wasafi kwa kosa la kurusha maudhui yasiyo na staha yaliyokashifu na kuleta tafsiri potofu kuhusu imani ya dini ya Kikristo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Hans Gunze, alisema maudhui yaliyorushwa na Wasafi kupitia mtandao wake wa ‘Youtube’, yenye kichwa cha habari ‘hata Yesu alifuata wenye pesa msituite matapeli.

“Baada ya kutafakari kamati imeridhia pasipo shaka kwamba kampuni ya Wasafi Televisheni kupitia kipindi chake kilichokuwa na kichwa cha habari cha hata Yesu aliwafuata wenye pesa msituite matapeli imekiuka kanuni za mawasiliano na kieletroniki na posta, maudhui ya mtandaoni za 2020 kama ilivyowasilishwa katika tathmini ya kamati,” alisema Gunze.

Gunze aliongezea kwakusema kipindi hicho kilitangazwa kupitia mtandao wa Youtube ya Wasafi Novemba mosi mwaka huu na mtangazaji, Jordan Mwasha (Mchaga og) ambaye alikuwa akifanya mahojiano na mtu anayejiita Nabii Daniel Shillah huku akisema kwamba Kamati ya Maudhui ya TCRA imebaini Wasafi imetenda kosa hilo kwa makusudi kwa kutangaza maudhui ya upotoshaji uongo, kukashifu, kukufuru na kutoheshimu imani.

Aidha, TCRA imetoa onyo kali na kukiamuru kituo hicho kuomba radhi watazamaji wake na umma kwa ujumla kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Desemba 23 hadi 25 mara tatu kwa siku kila baada ya saa nne na pia kuwakumbusha kujitathimini kwa kuwa ni dhahiri watanzangaji wake hawafahamu sheria na kanuni za utangazaji.

error: Content is protected !!