Pepsi na Coca Cola zaadimika mtaani

HomeKitaifa

Pepsi na Coca Cola zaadimika mtaani

Baadhi ya wafanyabiashara jiji Dar es Salaam wamesema kwamba soda zinazotengenezwa na kampuni za  Pepsi na Coca Cola zimeadimika kwa muda sasa tangu Desemba mwaka jana na kadri siku zinavyozidi kwenda upatikanaji wake umekuwa wa shida huku chanzo cha uhaba huo kikiwa bado hakijatajwa.

Baadhi ya wauzaji wa vinywaji wamaeeleza kuwa wafanyakazi wa kampuni hizo wamekuwa wakichukua oda zao kila siku lakini upatikanaji wake bado ni mgumu hivyo kufanya soda hizo kutokuwepo kabisa kwenye baadhi ya maduka.

Muuzaji wa jumla wa soda katika Soko la Vetenary, Dar es Salaam, Ally Mohamed alisema tangu Desemba mwaka jana, soda za Coca Cola ziliadimika na Pepsi zikawa inapatikana lakini hivi sasa hana soda za aina zote kutoka kampuni hiyo.

“Wafanyakazi kutoka kampuni hizo kama kawiada wanakuja kuchukua oda zetu lakini hatupati vinywaji, hivi sasa ninachouza hapa dukani ni maji pamoja na juisi mbalimbali,” alisema Ally.

Coca Cola huuza soda aina za Cocacola, Fanta, Sprite, Stone Tangawizi huku Pepsi ikizalisha soda ya Pepsi, SEven Up na Mirinda.

 

Habari Leo

error: Content is protected !!