Mpango: Mrema alikuwa kiongozi mkweli na mzalendo

HomeKitaifa

Mpango: Mrema alikuwa kiongozi mkweli na mzalendo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika salasala Jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole na kuifariji familia, ndugu , jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo aliyefariki tarehe 21 Agosti 2022 katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Makamu wa Rais amesema Marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi. Amesema taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.

error: Content is protected !!