Sensa ni siku 7 tunaomba uvumilivu

HomeKitaifa

Sensa ni siku 7 tunaomba uvumilivu

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda amesema wananchi watahesabiwa kwa siku saba hivyo wananchi ambao hawakufikiwa na makarani jana wasichoke kusubiri.

Makinda alisema hayo jana katika IKulu ya Chamwino Dodoma, muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumaliza kutoa taarifa kwa karani wa sensa.

Alisema makarani wa sensa jana wasingeweza kuzifikia kaya zote kwenye maeneo waliyopangiwa hivyo wangeifanya kazi hiyo kwa asilimia 15 tu hivyo wananchi wawe wavumilivu.

“Tungekuwa nchi iliyoendelea kila mtu angejisensa mwenyewe kwa kutumia simu yake, tunaomba sana malalamiko mengine haya msingi, karani hataweza kufika kila nyuma leo (jana) hii tunaenda mpaka siku saba kwa hiyo tuombe uvumilivu,” alisema Makinda.

Alishauri wananchi watumie maswali yaliyotolewa kuacha taarifa nyumbani na kwamba makarani wanaweza kupiga simu kuomba ufafanuzi.

“Kaya inaweza kuwa na fomu, ikajazwa mule ndani kama una kazi yako au unaenda kazini kwako taarifa unaiacha nyumbani. Karani akifika anaweza akatumia ile lakini akikuta hajapata uelewa vizuri atatumia simu uliyoweka, atakupigia kwamba tupo nyumbani kwako hatujaelewa au anaweza kukwambia kesho tutakuwa nyumbani kwako,” alisema Makinda.

error: Content is protected !!