Yafahamu mambo 6 yatakayochunguzwa na Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani

HomeKitaifa

Yafahamu mambo 6 yatakayochunguzwa na Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani

Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka huu, imeweka wazi maeneo sita itakayofanyia kazi kwenye uchunguzi wake.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman Chande wakati wa mkutano wake na wahariri nchini na kutaja mambo hayo ni kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha matukio, wakati wa uchaguzi huo na baada ya uchaguzi.

“Kuchunguza lengo lililokusudiwa na wale ambao tutaona walikuwa wamepanga na kutekeleza vitendo hivyo yaani lengo lao,” amesema na kutaja eneo lingine kuwa ni:

“Kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo majeruhi uharibifu wa mali na madhara ya kiuchumi na kijamii.”

Pia amesema watachunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali na vyombo vyake na mtu yeyote mwingine.

Amesema pia watapendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongoz na raia kwenye kulinda amani ya nchi, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria na kufikia maridhiano ya kitaifa.

Mwenyekiti huyo amesema pia watachunguza jambo lolote ambalo tume itaona ni muhimu na litaendana na majukumu ya tume.

error: Content is protected !!