Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema serikali chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan imetenga zaidi ya shilingi bilioni 100 na tayari wameshapokea bilioni 45 kwa ajili ya kutekeleza mchakato wa kuwa na mfumo wa anwani ya makazi yaani Postikodi.
Mchakato wa kuwa na anwani ya makazi utarahisisha mambo mengi katika sekta mbalimbali huku pia ukitarajiwa kusaidia wafanyabiashara katika kupeleka mizigo kwa wateja. Mfumo huo pia utarahisisha utendaji wa shughuli za kiserikali na kijamii pamoja na kurahisisha utambuzi wa watanzania waliopo na mahali walipo.