Zaidi ya Sh. Bilioni 100 kuboresha vyuo vya ufundi stadi

HomeKitaifa

Zaidi ya Sh. Bilioni 100 kuboresha vyuo vya ufundi stadi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inawekeza zaidi ya Sh bilioni 100 kwa ajili ya kuboresha elimu kwenye vyuo vya ufundi na stadi mbalimbali pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi kwenye vyuo hivyo.

Majaliwa amesema hayo jana Machi 12, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa upokeaji wa maombi kwa ajili ya programu endelevu ya uwezeshaji inayolenga kukuza wajasiriamali vijana wenye ubunifu na wanawake.

Ameeleza kuwa serikali imeendelea kuviwezesha vyuo vyake vya stadi mbalimbali kama VETA ili Watanzania wengi wapate nyenzo ya kupambana na umasikini.

Amesema miongoni mwa miradi ya kuboresha sekta ya elimu ni mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo ameeleza kuwa Sh trilioni 1 zitatumika kunufaisha zaidi ya wanafunzi milioni 6.5 hadi utakapokoma mwaka 2025.

error: Content is protected !!