WANANCHI zaidi ya 18000 wa kata sita za Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera waliokuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na salama utakaogharimu Sh bilioni 3 hadi kukamilika.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) Mhandisi Daudi Beyanga amesema kuwa mradi huo katika utekelezaji wake umefikia asilimia 92.
Baadhi ya wananchi wa kata hizo akiwemo Denice Kalugendo na Plasidia Alkadi wamesema kuwa mradi huo unaenda kutatua changamoto ya maji kwani wamekuwa wakifata maji umbali mrefu ambayo pia huchafuliwa na mifugo.
Ujenzi wa mradi huo wa upanuzi wa mtandao wa maji kwa Manispaa ya Bukoba unaotekelezwa kwa awamu mbili, ulianza kutekelezwa Desemba 2020 na unatarajia kukamilika Desemba 2024.