Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya zahanati 1,158 zimejengwa na kusajiliwa na zinatoa huduma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange alitoa kauli hiyo akijibu swali la Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda aliyetaka kujua, lini zahanati za Molemlimani, Muungano, Urafiki, Isanjandugu, Iyombakuzova na Kapumpa zitakamilika.
Alisema serikali imeendelea kujenga vituo vya kutolea huduma na kuivsajili ili vianze kutoa huduma za afya. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya zahanati 1,158 zimejengwa na kusajiliwa na zinatoa huduma.
Alisema katika mwaka wa fedha 2026/2027, serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge itatenga sh milioni 250 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati za Muungao, Urafiki, Isanjandugu, Iyombakuzova, Kapumpa na Molemlimani.