Mauzo albam ya  R Kelly yaongezeka

HomeBurudani

Mauzo albam ya  R Kelly yaongezeka

Mauzo ya albamu  ya R. Kelly yameongezeka kwa asilimia 517%, na uhitaji wa albamu hiyo kwa mwaka 2021 ni milioni 6.4, licha ya Septemba 27 mwanamuziki huyo kukutwa na hatia kwa makosa ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na watoto.

Mashabaiki wa R Kelly wameendelea kumfuatilia na kutafuta nyimbo zake licha ya kushitakiwa na kukutwa na hatia ya makosa hayo. Hivi karibuni Youtube imefuta akaunti za R Kelly hivyo ukihitaji kupata nyimbo zake zimebaki sehemu nyingine kama Spotify, Apple Music na Tidal.

> Youtube yafunga akaunti zote za R. Kelly

R Kelly amewahi kutuhumiwa kwa makosa yanayoendana na unyanyasaji wa wanawake na watoto tangu mwaka 2002 baada ya kuvuja kwa mkanda wa ngono za watoto pamoja na mkanda mwingine ukimuonesha akifanya ngono na mtoto chini ya umri, na ilipofika 2008 hakukutwa na hatia kwenye makosa yote hayo.

error: Content is protected !!