Mwaka 2013, Bara la Afrika lilikuwa linaongoza kwa kukua haraka kiuchumi kwa asilimia 5.6%, ambapo ni kiwango cha juu kuliko bara lolote kwa wakati huo. Hii kiuchumi ina maanisha kwamba, utawekeza leo barani Afrika kwenye sekta mbalimbali, basi uwezekano wa kupata faida kubwa zaidi miaka kadhaa ijayo ni mkubwa zaidi.
Watu wengi wenye asili ya Afrika waishio ughaibuni wana ari ya kutaka kuja kuwekeza barani Afrika, lakini hofu yao ipo kwenye mambo makubwa mawili, moja ikiwa ni machafuko ya kisiasa na mbili ni kutokufahamu vizuri sekta za uwekezaji.
Kuna fursa nyingi sana kwenye sekta ya uwekezaji barani Afrika, kufanya maamuzi ni sekta gani uwekeze inaweza ikawa changamoto. Lakini kutokana na utafiti na uchunguzi uliofanywa, tukutoe hofu kuwa zipo sekta ambazo uwekezaji wake unatoa mafanikio ya haraka sana barani Afrika.
1. Kilimo
Asilimia 25% ya ardhi yenye rotuba duniani iko Afrika, na kilimo kinachangia 15% ya mapato ya serikali zote barani Afrika. Licha ya Afrika kuwa na 25% ya ardhi yenye rotuba duniani, ardhi inayotumika kwa kilimo ni chini 10%, Utafiti unaonesha kwamba ili Afrika iendane na kasi ya dunia kwenye kilimo cha uwekezaji, basi trilioni 115 zinatakiwa kuwekezwa.
2. Nishati
Zaidi ya 50% ya watu barani afrika hawana umeme wa uhakika kwenye makazi yao, sekta ya nishati ni moja ya sekta ambazo zinatija sana barani Afrika. Bara la Afrika limebarikiwa fursa nyingi sana za uwekezaji katika sekta ya nishati, hasa katika uzalishaji wa nishati jadidifu, kwa kuwa bara la Afrika jua linawaka muda mrefu na katika maeneo mengi.
3. Sekta ya Fedha
Sekta ya Kifedha kupitia Benki ni sekta inayokua kwa kasi sana Barani Afrika. katika muongo mmoja uliopita, benki zilizopo katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara zinamiliki rasilimali zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 na Afrika Kaskazini ni shilingi trilioni 1.1
4. Bidhaa ndogo ndogo za viwandani
Hapa tunazungumzia vitu kama viberiti, soda, vyakula vya kusindika, sabuni na kadhalika. Matumizi ya bidhaa kama hizi yameongezeka sana barani Afrika, kuanzia 2005 hadi 2008 matumizi yamekua kwa zaidi ya 16%. Kwa mfano nchini Nigeria matumizi ya majumbani kutoka mwaka 2000 – 2005 yalipanda kutoka milioni 2 hadi shilingi milioni 9.
5. Uchimbaji wa Madini
Bara la Afrika lina utajiri wa madini kama Almasi, Platinum, Chromium, Gold, bauxite, cobalt na kadhalika. Madini yote haya yanahitaji kwa kiasi kikubwa na kwa matumizi mbalimbali duniani kote. Licha ya Afrika kuwa madini mengi sana, lakini bado kuna changamoto kwa nchi hizi kwenye kuyachimba na kuyaongezea thamani. Ukitaka kuwekeza barani Afrika, basi ni vyema ukazingatia maeneo yenye madini zaidi, mfano 88% ya madini ya Platinum iko Afrika ya Kusini 84% ya madini ya Chromium yanapatikana ukanda huohuo.
> Ajira rasmi 10 zinazolipa zaidi nchini Tanzania
6. Miundombinu
Sekta ya miundombinu Afrika imekuwa kutoka shilingi trilioni 7 mwaka 1998 hadi trilioni 32 mwaka 2008, ni sawa na 17% ndani ya miaka 10. UNMD ya Marekani inaripoti kwamba Kusini mwa Janga la Sahara kunahitaji uwekezaji wa miundombini yenye thamani ya shilingi trilioni 415. Hapa ni miundombinu ya barabara, bandari, magari na kadhalika.
7. Mawasiliano
Watumiaji wa simu barani Afrika wameongezeka kufika milioni 400 na mahitaji yamekuwa yakiongezeka kwa kasi zaidi ndani ya miaka mitano. Ili kukimbizana na kasi ya mahitaji, basi uwekezaji wa dola trilioni 34 unahitajika kila mwaka na unaweza kupata ongezeko la 50% la wateja wapya hasa kutoka vijijini.
8. Mafuta na Gesi
Afrika ina hazina kubwa ya gesi na mafuta. Mwaka 2015, 13% ya mafuta duniani yalizalishwa Afrika na uzalishaji unakua zaidi kila uchwao. Nchi 19 Barani Afrika zina rasilimali ya mafuta na gesi.
9. Sekta ya Afya
Afrika kuna uhaba mkubwa wa madaktari, hospitali hata vifaa tiba. Kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba au hospitali unaweza kupata faida kubwa sana. Shirika lisilofanya biashara la Bill and Melinda Gates Foundation hutoa trilioni 5 kila mwaka barani Afrika kusaidia katika sekta ya afya. Lakini bado Afrika kuna matatizo makubwa sana katika sekta ya afya.
10. Elimu
Zaidi ya 50% ya watu wote barani Afrika wana umri chini ya miaka 31, na ni 6% ya ya watoto barani Afrika ndio hupata fursa ya kusoma shule. Afrika ina watu werevu sana, lakini watu hawa wanapata shida kupata sehemu za kusoma na kukuza vipawa vyao. Kujenga shule au vyuo vyenye vifaa vya kisasa kutakupatia faida kubwa sana kwani uhitaji ni mkubwa sana.
Chanzo: African Vibes