Zingatia mambo matano mara zote upandapo Uber, Bolt

HomeBiashara

Zingatia mambo matano mara zote upandapo Uber, Bolt

Tatizo la usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam limekuwa kero kwa kipindi kirefu sana na hii ni kwa sababu ya foleni na ukosefu wa daladala hasa nyakati za jioni na asubuhi, ndipo kampuni za uchukuzi za Uber na Bolt lilipochukua jukumu la kutoa huduma za usafiri.

Kutokana na changamoto hiyo ya usafiri, Uber na Bolt zimekuwa wakombozi kwa wakazi wa Dar es Salaam kwani zinatoa huduma kwa nusu bei ya taxi za kawaida. Hivyo basi kwa wakazi wa Dar es Salaam yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia unapotumia Uber, Bolt au usafiri unaofanana nao.

1.Zingatia vigezo na masharti ya huduma hiyo
Hakikisha unasoma masharti na vigezo kabla ya kuanza kutumia app yoyote ile, kwani kukubali masharti na vigezo ina maanisha kwamba umeingia mkataba na mtoa huduma huyo. Mfano Ukiomba Uber na dereva akafika na kuanza kukusubiri hadi zaidi ya dakika 10 kisha ukaihirisha safari utachajiwa gharama za ziada zitakazokuwa deni. Deni hilo litajumuishwa utukapoomba usafiri huo hapo baadaye.

2. Kuwa na nauli ya ziada na makadirio ya App
Mfano umeita Uber ikasoma shilingi 1000 hakikisha unakuwa na pesa ya ziada kwani nauli  inaweza kuongezeka wakati mwingine kutokana na umbali wa sehemu uendapo au foleni.

      > Zijue faida za kula chakula cha usiku mapema

3. Kaa kiti cha nyuma
Kwa usalama wako upandapo Uber au Bolt hakikisha unakaa kiti cha nyuma ili iwe rahisi kujiokoa pale tatizo linapotokea. Nyuma kuna milango miwili kwahiyo unaweza kutoka pande yoyote tofauti na unapokaa mbele kwani upande wa kulia ni kiti cha dereva.

4. Hakikisha ramani ya unapokwenda
Unapoita Uber au Bolt hakikisha unaweka ramani sahihi ya sehemu unapokwenda au kama haipo kwenye ramani weka eneo la karibu na hapo uendapo. Kwa wale ambao app hujiweka eneo la mwisho ulilokuwepo, ni vyema kuhakikisha sehemu unayoomba uchukuliwe ni pale ulipo kwa kuangalia kwenye ramani huku GPS ikiwa imewashwa.

5. Acha ubosi
Kumbuka ile ni Uber/Bolt na sio usafiri wako binafsi hivyo jaribu kuwa mstaarabu ukiwa ndani ya gari. Ni dhahiri kuwa unahitaji huduma lakini jaribu kuwa mstaarabu uwapo ndani ya usafiri wa aina hii. “Washa AC”, “weka reggae”, “ongeza sauti mpaka mwisho,” epuka ubosi usio wa lazima.

Uber na Bolt ni wakombozi kwa usafiri wa haraka na wa muda wote ila manufaa yataonekana zaidi iwapo wote madereva na abiria watazingatia taratibu muhimu ili kuongeza mahusiano na kukuza biashara.

error: Content is protected !!