kwa vijana wengi kupika ni mtihani mkubwa kwao muda, muda unaotumika kupika unaweza kutumika kufanya mambo mengine, hivyo mtu huamua kununua chakula cha haraka na kula. Tabia hii inaweza kumgharimu mtu kwa namna mbalimbali ambazo zitaelezwa hapo chini. Si kwamba tunakataza watu kununua vyakula vya fast food, lakini ni bora mtu kuzingatia zaidi usafi wa maandalizi wa vyakula hivyo kwani yawezekana yapo mambo yanayojiri mbali na upeo wa macho yetu.
Vitu gani sasa vinaweza kuzingatiwa kabla ya kununua ‘Fast Foods’.
1. Uandazi mbaya wa vyakula
Ni kweli unaweza kuogopa kumuona muuza chakula akiwa anaandaa chakula huku nywele za zikiwa timtim na hazijafunikwa, anazungumza kwakutumia nguvu huku ameshika chakula chako, unaweza usinunue kabisa kutokana na mazingira hayo. Fast Foods nyingi wanajitahidi kutengeneza vyakula katika mazingira nadhifu, wakiongozwa na sheria za nchi katika kufanya shughuli hiyo. Lakini je, mamlaka husika kwa maana ya serikali, imejiridhisha kweli katika hukakisha sheria za usafi katika uandaza wa vyakula unafuatwa? Hili ni suala la kutazama
2. Uchaguzi mbaya wa lishe
Kutokana na ufinyu wa machaguzi ya vyakula, hatari ya kuchagua chakula kisichozingatia lishe bora ni mkubwa zaidi. Vyakula vya haraka (fast foods) vingi vinasifa ya kutokuwa na lishe bora endapo vitatumika kwa wingi. Kutokana muda kuwa mchache, watu wengi wameangukia kula vyakula ambavyo kimsingi havishauri sana kwa afya. Kula lishe bora kuna hitaji shughuli kidogo, kwani kunaweza kumlazimu mtu apike kile anachopenda katika mazingira safi na uwanda mpana wa kufanya machanguzi.
3. Matumizi mabaya ya fedha
Vyakula vya fast food ni ghali kwa maisha ya kijana au mtu wa kawaida. Kama manunuzi yako ya fast foods sio mara kwa mara, inaweza kuwa ngumu kwa mtu kuanza kuhisi gharama. Lakini kwa wale watumia vyakula hivi mara kwa mara, gharama ni kubwa kulik kupika mwenyewe.