199 namba mpya ya huduma kwa wateja

HomeKitaifa

199 namba mpya ya huduma kwa wateja

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuujulisha Umma kuwa, katika kuboresha huduma zake za mawasiliano, unabadilisha namba ya simu bila malipo katika kituo cha Huduma kwa Wateja kutoka namba 0800 110063 kuwa namba 199.

Namba 199 ya bila malipo itaanza kutumika rasmi kuanzia Julai 1,2022 na huduma zitaendelea kutolewa kwa saa 24 siku 7 za wiki kama ilivyo sasa.

Mfuko unawahakikishia wadau wake kuwa utaendelea na ushirikiano wake wakati wowote wadau watakapohitaji msaada kupitia kituo hicho.

error: Content is protected !!