300 wakamatwa kwa kutotumia daraja la watembea kwa miguu

HomeKimataifa

300 wakamatwa kwa kutotumia daraja la watembea kwa miguu

Watu zaidi ya 300 wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kwa kosa la kutotumia daraja la juu la watembea kwa miguu lililowekwa kwa ajili ya  kuvukia  barabara na badala yake wao kuvuka kwa kukatisha barabara kinyume na utaratibu.

Kama ulikua unahisi watumiaji wa vyombo vya moto peke yake wanatakiwa kufuata sheria na alama za barabarani basi hauko sahihi kwani watumiaji wote wa barabara wanatakiwa kufuata sheria za barabarani ikiwemo kupita kwenye sehemu sahihi zilizowekwa.

Polisi wanasema vifo vinavyotokana na ajali ni vingi na asilimia 40 ya watu wanaogongwa na kupoteza maisha ni watembea kwa miguu. Kwa takwimu hizo Serikali inataka kupunguza vifo na madhara yanayotokana na ajali kama kilema cha kudumu ambacho kinafanya mtu kuwa tegemezi maisha yake yote, ongezeko la watoto wa mitaani baada ya kupoteza wazazi na msongo kwa wenza au ndugu baada ya kufiwa.

Watu waliokamatwa kutokana na kosa hilo walitakiwa kulipa faini ambayo ina thamani sawa Shilingi ya Tanzania 10,000 hadi 62,000 na walioshindwa kulipa walipelekwa kituo cha Polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Kwa unavyowafahamu ndugu zetu Watanzania, unadhani kama ukamataji huu ungefanywa hapa nchini ni watu wangapia wangematwa kwa kuvuka barabara sehemu ambazo hazistahili?.

error: Content is protected !!