Waziri Mkuu azuru eneo la mauaji ya Mbunge

HomeKimataifa

Waziri Mkuu azuru eneo la mauaji ya Mbunge

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson leo Jumamosi amezuru eneo ambalo Mbunge wa Chama wa Wahafidhina, Sir. David Amess amechomwa kisu na kufariki siku ya jana tarehe 15 Oktoba 2021 wakati akifanya mkutano jimboni mwaka Essex.

Waziri Mkuu kwenye ziara hiyo ya heshima ya kuweka mashada kwenye eneo la mauaji ya Mbunge huyo, ameongozana na kiongozi wa Chama cha Labour, Keir Starmer na Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Priti Patel.

> Mbunge auawa kwa kuchomwa kisu

Uchunguzi wa awali wa Askari unaonesha kuwa tukio hilo linahusishwa na tukio la kigaidi ambalo linahisiwa kutekelezwa Waislamu wenye itikadi kali. Mauaji ya Sir. David, yametokea miaka mitano baada ya mauaji ya Mbunge mwingine wa Chama cha Labor, Jo Cox mwaka 2016. Matukio haya mawili yameibua mjadala wa kupitia upya itifaki za ulinzi kwa wabunge nchini Uingereza.

error: Content is protected !!