76% ya Watanzania hawapigi mswaki

HomeKitaifa

76% ya Watanzania hawapigi mswaki

Asilimi 76.5 ya Watu wazima Tanzania wameoza meno kutokana na kutopiga mswaki.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kinga na Meno kutoka Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzoba amesema watoto walioza meno nchini ni asilimia 31.1

Amesema sababu kubwa ya tatizo la kulegea, kutoboka na kuoza kwa meno linalowakabili watoto na watu wazima katika jamii ni kutopiga mswaki vizuri ikiwa ni Pamoja na matumizi ya sukari iliyosindikwa inayopatikana katika vyakula mbali mbali.

“Kawaida mtu anapaswa kupiga mswaki angalau mara mbili kwa siku, asubuhi anapoamka na usiku anapotaka kulala, sasa watanzania wengi kupiga mswaki inaonekana ni kipengelee, wengi wanapata matatizo ya kinywa kwa kutopiga mswaki.”Amesema

Kauli ya Dk Nzoba imekuja baada ya Shirika la Afya Dunia (WHO), kutoa ripoti yake juzi Novemba 20, 2022 inayooneysha karibu nusu ya watu duniani sawa na asilimia 45 au watu bilioni 3.5 wanaugua magonjwa ya kinywa, huku watu 3 kati ya 4 walioathirika wakiishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Kwa mujibu wa WHO magonjwa ya kawaida ya kinywa ni kuoza kwa meno, ugonjwa ya fizi, kupoteza meno na saratani ya mdomo.

 

error: Content is protected !!