Mapya yaibuka ajali ya ndege ya Precision Air

HomeKitaifa

Mapya yaibuka ajali ya ndege ya Precision Air

Ripoti ya awali ya ajali ya ndege ya Precision iliyotokea eneo la Ziwa Victoria imeonyesha kwamba mfanyakazi mmoja wa ndege hiyo akishirikiana na abiria ndio waliofungua mlango wa ndege na kuwezesha abiria wengine kutoka.

Katika ripoti hiyo inaleza kwamba kikosi cha maji cha uokoaji kilipata taarifa dakika 15 baada ya ajali hiyo kutokea na walipofika eneo ya tukio walishindwa kufanya uokoaji kutokana na ukosefu wa oksijeni kwenye mitungi yao.

‘’ Boti ilifika saa saba eneo la tukio, baada ya kufika walikua na changamoto ya kuishiwa mafuta na oksijeni, kabla hawajafika, mvuvi mmoja tayari alianza kutoka maiti zilokua ndani ya ndege’’ taarifa ya ripoti inasema.

Taarifa ya ripoti hiyo pia haijatoa sababu kamili ya nini kilisababisha kutokea kwa ajali, ikisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania awali ilibainisha kuwa baada ya ripoti ya awali itafuatia ripoti ya uchunguzi wa awali inayotarajiwa kuchapishwa mwezi mmoja baada ya ajali na kisha ripoti kamili baada ya mwaka mmoja.

AIB BULLETIN ACC 6-22 5H-PWF 21 November 2022 (1_221122_122008

error: Content is protected !!