Rapa kutoka nchi Marekani Ye au Kanye West amefutwa kwenye orodha ya wasanii wanaotarajia kutumbuiza kwenye Tuzo za Grammy 2022 kutokana na matendo yake ya mtandaoni baada ya kumwambia maneno yaliyoashiria ubaguzi wa rangi kwa Mchekeshaji na mtangazaji Trevor Noah ambaye anatarajiwa kuwa mshereheshaji siku hiyo ya tuzo.
Hii imetokea baada ya Trevor Noah kuandika kwenye mtandao wa Instagram kwamba Kanye ana msumbua aliyewahi kuwa mke wake Kim Kardashian na ndipo Ye akamjibu kwa kutumia maneno ya wimbo wake ambayo ni yakibaguzi.
Baada ya kumjibu Noah, hatua hiyo ilisababisha usimamizi wa Instagram ambao ni kampuni ya Meta impige marufuku ya saa 24 na kuondoa baadhi ya maneno aliyoandika.