Kwenye karne hii ambayo teknolojia imekua na watumiaji pia wamekua wengi, watu hupenda kujifunza vitu mbalimbali kupitia mitandao hasa Youtube ambapo huangalia jinsi yakufanya au kuona namna vitu vinavyofanyika.
Wasichana wengi wamekuwa wakiingia Youtube na kujifunza urembo mbalimbali hasa wa uso ili waweze kupendeza lakini kuwa makini na somo unalolipata kwani sio kila kitu kinasaidia na kumbuka sura yako ndio utambulisho wako.
Usipake vitu hivi usoni;
Dawa ya meno
Vipindi vingi vya youtube vinavyohusu urembo vinashauri watu kupaka dawa ya meno usoni kwa kuwaaminisha kwamba inaondoka vipele, sio kweli na kamwe usijaribu kupaka dawa hii usoni kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi kutokana na vitu vilivyotumika kutengenezea dawa hiyo.
Soda ya kuoka (Baking Soda)
Kwa akili tu ya kawaida, hii hutumika kwenye kupikia maandazi au keki na unaona kinachotokea alafu bado unaweka usoni. Usipake usoni kwa sababu wewe sio chakula.
Rangi za kucha
Rangi hizi hutengezwa kwa kemikali kali sana hivyo siyo salama kupaka usoni kwani inaweza kukusababishia madhara makubwa zaidi.
Usipake mkojo
Kuna baadhi ya watu wanadiriki kupaka haja ndogo usoni wakiamini kwamba watakua na ngozi laini kitu ambacho sio kweli na unapaswa kuachana na dhana hii potofu.