Vita ya Ukraine na Urusi ambayo bado inaendelea imeitikisa dunia kwa kiwango kikubwa huku nchi, na kampuni mbalimbali zikichagua upande wa kuegemea kati ya Ukraine na Urusi, lakini kwa Afrika hali ni tofauti.
Nchi nyingi za Afrika zimeamua kutokuchagua upande wa kuegemea kwenye vitahii kwa sababu mbalimbali ikiwemo zifuatazo.
Umoja wa mataisha uliitisha kura wakiwataka Urusi kuondoa majeshi yake Ukraine, kati ya nchi wanachama 193, nchi 141 zilipiga kura za ndio kukubali azimio hilo, nchi 5 zikapiga kura za hapana.
Kati ya nchi 54 za Afrika, Eritrea ndio nchi pekee iliyopiga kura ambayo ilikuwa ya hapana. Nchi 16 zilichagua kutokuchagua upande wowote huku nchi 9 hazikupiga kura kabisa. Hivyo zaidi ya nusu (nchi 26) zilichagua kukaa nje ya vita hivyo.
Nchi nying za Afrika zinaonekana kuwa na wasiwasi juu ya dhamira ya NATO. Baadhi ya nchi zikisema NATO ingeweza kusaidia kuepusha vita hiyo mapema kabla ya maafa kuanza.
Mwaka 2012 NATO ilihusika na kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gadaffi baada ya kuivamia Libya huku nchi hiyo ikitaka NATO iwajibishwe kwa kitendo kile na baadhi ya nchi bado hazikubali kitendo kile.
Sababu nyingine ni kwamba baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia, Mali na Libya wamekuwa na mashirikiano ya kijeshi na Urusi na wengine kupata misaada wawapo kwenye mashambulizi.
Mwaka 2014 Marekani waligoma kuwauzia baadhi ya silaha Nigeria wakipigana na Boko Haram kwa sababu walizosema ni kinyume na haki za binadamu hivyo Nigeria kulazimika kupata msaada kutoka kwa Urusi.
Urusi iliingia makubaliano na Nigeria pamoja na Ethiopia mwaka jana ya kushirikiana kijeshina imekuwa ikizisaidia nchi za Afrika kwa zana za kivita.
Nchi nyingi za Afrika pia zinaitegemea Urusi kwa ngano. Kwa miaka miwili kati ya 2018 na 2020 Urusi na Ukrainne waliingiza ngano Afrika zenye thamani ya takribani $5.1bn.
Vilevile kuonekana kwa ubaguzi na kutokupata ushirikiano mzur kutoka kwa nchi za Ulaya na Marekani kipindi cha kupambana na janga la UVIKO kumezifanya nchi nyingi za Afrika kufikiria tena uhusiano wao na nchi hizo. Kwani ni ukweli usiopingika kuwa nchi zilizoendelea hujipendelea wenyewe kabla ya kuwaza nchi za chini ambazo nyingi ni za Afrika.
China ambayo ni mbia mkubwa wa nchi nyingi za Afrika naye aliamua kukaa kando hivyo ikaonekana ni sawa kwa nchi zinazokubaliana na China kufuata mrengo huo.
Mwisho, Afrika imekuwa ikiathirika na vita mbalimbali zilizotokea duniani. Hivi sasa vita ya Ukraine na Urusi imesababisha kupanda kwa bei za mafuta Afrika na vilevile kukosekana ka baadhi ya vitu kwa idadi stahili ikiwemo kukosekana kwa ngano.
Waafrika bado wanakumbuka athari za vita kuu za dunia na Vita baridi kwa Afrika igawa hawakuhusika na ikiwa si miaka mingi tangu nchi zote za Afrika kupata uhuru, bado Afrika ingependa kuendelea kufurahia uhuru wake bila kujiingiza kwenye chochote kitachopelekea uhuru na amani kuharibika.