Mwanamke kulia wakati wa kujamiiana ni sawa?

HomeElimu

Mwanamke kulia wakati wa kujamiiana ni sawa?

Mwanamke kulia wakati wa kujamiiana ni sawa?

Kwa wengi tendo la ndoa ni tendo la kihisia na lenye kuleta furaha na ukaribu baina ya wawili hao ambapo wakati mwingine hupelekea hisia za kupitiliza na mtu kufanya jambo ambalo hakuwa akitegemea.

Baadhi ya wanaume hujikuta matatani wasijue nini cha kufanya baada ya wapenzi wao kuanza kububujikwa na machozi katikati ya tendo huku mwanamke akijitafakari kwanini analia na pengine kuhisi ana shida.

Ni sawa na ni kawaida kwa hali kama hiyo kutokea yawezekana ukalia kwa sababu mbalimbali kwani mwili wako unakuwa hauna uwezo wa kuzuia hisia hizo.

1. Una furaha
Hii ni mojawapo ya sababu ya wanawake wengi kutokwa machozi wakati wa tendo la kama ilivyo kwa mtu kulia kwa furaha pale anapopewa zawadi nzuri bila kutarajia.

2. Una huzuni
Pengine kuna mambo ya nyuma yalikukwaza na hukupata wakati wa kuyaachia na hivyo wakati wa tendo la ndoa mwili, na akili vikafikia sehemu ya kujiachia na kuonesha huzini iliyokugubika. Inaweza kusaidia kupunguza huzuni lakini pia ni vyema kufanyia kazi chanzo cha huzuni ili hali hiyo isijirudie.

3. mabadiliko ya homoni
Homoni zinazoachiliwa na mwili wakati wa kujamiiana ni ‘dopamine’ na ‘oxytocin’ ambazo huachia hisia za furaha na utulivu. Wakati homoni hizo zikiachiliwa mwilini kwa wingi mwili unaweza kushindwa kujua nini kinafuata na kupelekea macho kujaa machozi.

4. Akili na mwili vyote vinashiriki kikamilifu kwenye tendo
Unapokuwa umetuliza akili na kuruhusu hisia zako kuwepo kikamilifu kwenye tendo kunakufanya uweze kuhisi mihemko ya hisia mbalimbali ikiwemo kupokea hisi mpya kabisa.

5. Umefika kileleni
Kwa mwanamke kufika kileleni ipo mihemko ya hisia nyingi ambazo huja pia kwa viwango vikubwa na mapokeo na matokeo yake yakawa tofauti tofauti, wapo ambao huishia kupiga chafya, wapo ambao hupiga miayo, wengine hucheka na hata kulia yote ni sawa.

Endapo kulia kwako kutakua ni kwa mwendelezo na hakukupi amani ni vyema kuonana na mshauri wa masuala ya uzazi au mahusiano.

error: Content is protected !!