Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema hivi karibuni serikali itatangaza ajira 32,000 kwa sekta zenye uhaba wa watumishi.
Waziri Mhagama ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha pili cha mkutano wa saba wa Bunge la 12 na kuongeza kuwa rais Samia Suluhu Hassan ameafiki ajira hizo.
“Serikali ilipanga kuajiri watumishi 44,000 kwa mwaka huu wa fedha, na tayari tumeshaajiri watumishi 12,000 na sasa nitangaze kuwa wiki ijayo nitatangaza ajira 32,000,” amesema Mhagama akijibu maswali ya nyongeza ya wabunge waliotaka kufahamu namna Serikali itapeleka watumishi kuziba nafasi katika vituo vingi vilivyojengwa nchini.