Harmonize hakati tamaa

HomeBurudani

Harmonize hakati tamaa

Harmonize bado anazidi kuonyesha kutokata tamaa ya kumpata aliyewahi kuwa mpenzi wake, Kajala Masanja na sasa amemnunulia cheni za dhahabu zenye thamani ya shilingi milioni 5 huku akimuomba apokee zawadi hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Insta story, Harmonize ameweka video ikionyesha cheni hizo na maua pamoja na ujumbe wakumuomba Kajala amu-unblock ili aweze kuwasiliana naye vizuri.

Hivi karibuni mmiliki huyo wa lebo ya Konde Boy, amekuwa akionyesha kutaka kurudiana na Kajala kwa kukiri kwamba bado anampenda na amsamehe kwa kosa alilofanya mpaka wakaachana.

 

error: Content is protected !!