Watu wawili wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyohusisha gari dogo na malori mawili usiku wa kuamkia leo, muda wa Saa 4:40 usiku, Iringa.
Katika ajali hiyo iliyotokea Kijiji cha Rugemba, Mafinga, Mwanahabari mkongwe aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzani, Neville Meena alikuwa miongoni mwa wanusurika akitokea Njombe kuelekea Dar es Salaam.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Meena amesema haya;
Muda wa Saa 04:40 usiku huu tumepata ajali hapa katika Kijiji cha Rungemba, Mafinga mkoani Iringa. Tulikuwa tukitokea Njombe kikazi tukielekea D’Salaam. Tunamshukuru Mungu mimi na kaka yangu Jesse Kwayu tumetoka salama. Ajali pia imehusisha malori mawili na watu wawili wamefariki pic.twitter.com/hoBL1XbtcE
— Neville Meena (@NevilleMeena) April 14, 2022