Mwanaume mmoja raia wa Kenya amekutwa na hatia ya kumuua kikongwe wa miaka 81 kwa kumziba uso kwa mto, kosa lililopelekea kuhukumiwa kifungo cha maisha bila msamaha.
Billy Chemirmir (45) amehusishwa na vifo vya zaidi ya waze 20 nchini Marekani huku akipewa jina la “serial killer” kabla ya kukutwa na hatia ya kumuuua mzee huyo aliyejulikana kama Lu Thi Harris mwaka 2018.
Chemirmir anatajwa kufanya matukio hayo ndani ya miaka miwili wakati akifanya kazi katika nyumba za wazee na kuwaibia mali zao.
Katika kipindi chote hicho Chemirmir aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa hana hatia na hakutoa ushahidi mahakamani.
Chemirmir alikamatwa Machi 2018 baada ya Mary Bartel (91) kusema kuwa mwanamume mmoja alilazimisha kuingia katika nyumba yake kwenye makazi ya wazee huko Dallas na kupelekea polisi kumfuatilia Chemirmir aliyeishi kariu namakazi hayo na kumkuta na vito vilivyoibwa ikiwemo na anuani ya Harris aliyekutwa ameuawa chumbani kwake.
Wakili wa mshitakiwa, Kobby Warren alilitaka Baraza la waamuzi kufuata sheria kwani vielelezo havitoshi kuthibitisha kuwa Chemirmir ndiye muuaji.
Baraza hilo lilitumia dakika 45 kabla ya kutoa hukumu.