Mahakama moja magharibi mwa Ujerumani ilimpata mwanamke mmoja na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia na kumpa kifungo cha nje cha miezi sita kwa kuharibu kondomu za mpenzi wake kimakusudi, vyombo vya habari vya Ujerumani viliripoti.
Katika kutoa uamuzi huo, hakimu alisema kesi hiyo isiyo ya kawaida ilikuwa moja ya vitabu vya historia ya sheria za Ujerumani – inayowakilisha tukio la uhalifu “wizi,” lakini wakati huu ilitekelezwa na mwanamke.
Kesi hiyo ilihusu mwanamke mwenye umri wa miaka 39 ambaye alikuwa kwenye uhusiano wa “marafiki wenye manufaa” na mwanamume wa miaka 42. Wawili hao walikutana mtandaoni mwanzoni mwa 2021 na kuanza uhusiano wa kimapenzi wa kawaida.
Kulingana na ripoti, mwanamke huyo alikua na hisia za kina kwa mpenzi wake lakini alijua kwamba hakutaka kuwa katika uhusiano wa kujitolea.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 kisha alitoboa mashimo kwa siri kwenye kifurushi cha kondomu ambazo mpenzi wake alihifadhi kwenye meza yake ya kulalia. Alitarajia kupata ujauzito, lakini juhudi zake hazikufua dafu.
Licha ya hayo, baadaye alimwandikia mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 42 ujumbe kwenye WhatsApp, akisema kwamba aliamini kwamba alikuwa mjamzito – na kumwambia kwamba alikuwa ameharibu kondomu kimakusudi.
Mwanamume huyo kisha alimfungulia mashtaka ya uhalifu – na mwanamke huyo baadaye alikiri kujaribu kumdanganya mwenzi wake.