Tanzania yaongoza kuwa na Nyati wengi barani Afrika

HomeKitaifa

Tanzania yaongoza kuwa na Nyati wengi barani Afrika

Tanzania inatajwa kuwa nchi inayongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya nyati barani Afrika kwa kuwa na jumla ya nyati 191,805.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana, jana Novemba mosi, 2022 jijini Arusha, wakati akitangaza matokeo ya sensa ya wanyamapori iliyofanyika mwaka huu.

Waziri Chana amesema nyati hao wengi wanapatikana katika mifumo ikolojia ya Serengeti (69,075) Nyerere-Selous-Mikumi (66,546), Katavi-Rukwa (35,273) pamoja na Ruaha-Rungwa ( 20,911).

Lengo kuu la Sensa hiyo, ambayo hufanyika kila baada ya miaka mitatu katika mfumo Ikolojia ya Katavi –Rukwa na Ruaha-Rungwa ni kujua uwepo, idadi, mtawanyiko pamoja na viashiria hatarishi kwa ustawi wa wanyamapori nchini Tanzania.

Pia Dk Chana amesema idadi ya wanyama hao imeendelea kuongezeka hasa katika maeneo ya ndani ya hifadhi, ambapo nyati hao wameongezeko kwa asilimia 64 kutoka mwaka 2018.

error: Content is protected !!