LHRC: Spika yupo sawa kuhusu akina Mdee

HomeKitaifa

LHRC: Spika yupo sawa kuhusu akina Mdee

Afisa Uchehemuzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Maduhu William amefanya uchambuzi kuhusu maamuzi yaliyotolewa leo na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ya kwamba wabunge 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wataendelea kubaki bungeni mpaka pale mahakama itakapo toa tamko rasmi, ni sawa kikatiba na sheria.

“Mheshimiwa Spika ametumia ibara ya 107(A) kwa maana kwamba asingeweza kuchukua hatua ya kuwaondoa wabunge bungeni bila kujua mahakama itasema nini. Amedai kwamba hawezi kuchukua hatua anasubiri mahakama itazungumza nini na mahakama ndio itakua chombo cha mwisho kutamka kama Chadema walikosea utaratibu haukufuatwa wa kuwavua uanachama au utaratibu ulifatwa,” alisema Maduhu.

Maduhu alisema pia kwamba, maamuzi yaliyochukuliwa na Spika Tulia ni dhahiri kwamba ana heshimu mhimili mwingine kwa mujibu wa katiba.

Lini mahakama itamaliza kesi hiyo?

Bw. Maduhu alisema kwamba, mahakama ni taasisi huru na na inajiendesha kwa mujibu wa sheria na taratibu zake hivyo kumalizika kwa kesi hiyo ni mpaka pale muda ukifika wa kuanza kusikilizwa.

“Mahakama huwezi kuipangia kwamba kesi yako isikilizwe na iishe siku hiyo hiyo au ndani ya mwezi mmoja au miwili. Inategemea na upatikanaji wa majaji na hiyo kesi inakua kesi namba ngapi…kwahiyo suala la kwamba mahakama itamaliza lini hili suala tuiachie mahakama yenyewe kwa mujibu wa katiba na sheria kama chombo huru,” amesema Maduhu. 

error: Content is protected !!