Alichozungumza Prof. Lipumba na Rais Samia

HomeKitaifa

Alichozungumza Prof. Lipumba na Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kufika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Mei, 2022.

Profesa Lipumba amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuweza kukutana na kuzungumza pamoja kwani ni njia moja wapo ya kutekelezaji wa demokrasia katika nchini.

“Tumezungumza namna ya kujenga misingi mizuri ya demokrasia katika nchi yetu na yeye ametueleza nia yake dhabiti ya kuweza kuendeleza demokrasia katika nchi yetu na sisi hilo ndio lilikuwa kiu yetu,”

“La msingi yeye amesisitiza kwamba yeye ni muhumini wa demokrasia na anania dhabiti ya kujenga mifumo ya demokrasia na tuweze kuwa na uhuru wa kujadiliana, kuzungumza na kutoa maoni yetu.

Aidha, Profesa Lipumba amesema katika kikao hiko amejadiliana na Rais Samia Suluhu kuhusu umuhimu wa kufanya siasa za kistaarabu, kushindana kwa hoja pamoja na kumueleza Mhe. Rais umuhimu wa vyama vya siasa katika kukosoa serikali.   

error: Content is protected !!