Rais Samia ampa milioni 2 Mariam kwa kukumbatia watoto njiti

HomeKitaifa

Rais Samia ampa milioni 2 Mariam kwa kukumbatia watoto njiti

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25) anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huu umetumwa siku moja tangu mitandao ya Mwananchi Julai 18, 2023 iliporipoti habari kuhusu Mariam na namna alivyosaidia watoto watatu waliotelekezwa na mama zao.

Samia ametuma ujumbe huo leo Jumatano, Julai 19, 2023 uliwasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Brayson Kiwelu ambaye amemkabidhi Mariam kiasi cha Sh2 milioni.

Dk Kiwelu amesema ujumbe huo umetumwa na Rais Samia ambaye amekuwa mstari wa mbele katika huduma za mama na mtoto.

“Rais ametoa Sh2 milioni fedha taslim kumpatia mama huyu kwa kujitoa kwake na amewapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Amana kwa ubunifu huu na uthubutu mama huyu kuwa sehemu yetu.

“Rais ameshukuru sana msaada ambao mama huyu ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji,” amesema Dk Kiwelu.

SOURCE: MWANANCHI 

error: Content is protected !!