Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inawatangazia wananchi na wadau wote usafirishaji kuwa inaendelea na maboresho katika miundombinu ya barabara kwa kufunga mashine za kuhesabu magari kwenye baadhi ya sehemu za barabara za lami nchini. Mashine hizo kitaalamu zinaitwa “Inductive loop vehicle counters”.
Kazi kuu ya mashine hizo ni kuhesabu idadi ya magari yote yanayopita katika barabara husika kwa ajili ya matumizi ya kiofisi.
Tunawaomba wadau wa usafirishaji kufahamu kuwa, kazi ya mashine hizo si kupiga picha magari yanayoenda kwa mwendokasi.
TANROADS inaomba ushirikiano wa wananchi na wadau wote, katika ulinzi wa mashine hizo na kutoa taarifa kwa mameneja wa TANROADS wa mikoa au kituo cha polisi endapo watabaini hujuma yoyote.
Yeyote atakayebainika kufanya wizi au uharibifu katika mashine hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.