Alichosema Ruto baada ya ushindi

HomeKimataifa

Alichosema Ruto baada ya ushindi

Baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kumtangaza Dk William Ruto kuwa mshindi (Rais Mteule)  wa uchaguzi uliofanyika Agosti 9 mwaka huu, ametaja siri ya ushindi kwamba ni Mungu.

“Tuko hapa kwa sababu kuna Mungu wa Mbinguni. Nikiri tu kwamba bila Mungu tusingekuwa hapa. Asanteni wote mliopiga kura na tunawashukuru watu wa kenya kwa kuweka mfano.

“Uchaguzi huo ulihusu masuala mengi zaidi ya ukabila ambayo yamekuwa yakitawala uchaguzi mkuu. Ilikuwa ni kuuza ajenda na mipango yetu lakini sio ukabila,

“Katika uchaguzi huu hakuna walioshindwa. Wananchi wa Kenya wote wameshinda. Shujaa wa uchaguzi huu ni IEBC. Nasema hivi kwa uhakika, matokeo yote yalikuwa kwenye tovuti ya umma na hapa IEBC iliweka upeo,

“Niseme nitaongoza serikali ya uwazi na niko tayari kufanya kazi na watu wote akiwemo mpinzani wangu wa karibu Raila Odinga. Nimshukuru pia Rais Uhuru Kenyetta, Bosi wangu wa muda mrefu. Wale waliofanya mabaya dhidi yetu wasiwe na wasiwasi hatuna haja ya kushikana uchawi, tunahitaji kushirikiana pamoja,” amesema Rais Mteule Dk William Ruto aliyepata asilimia 50.49 ya kura akifuatiwa na Odinga aliyepata asilimia 48.8.

error: Content is protected !!